Friday, 27 January 2012

NINAVYOLICHAMBUA SAKATA LA MADAKTARI.



Kama mwananchi wa kawaida nimeguswa na mgomo huu wa madaktari wetu. Kwangu mgomo huu nautenganisha katika makundi matatu ambayo yote yanahusisha wadau wakubwa si katika mgomo tu bali sekta nzima ya Afya Nchini.

  • Madaktari
  • Serikali
  • Wagonjwa
MGOGORO
Mgomo ni wa madaktari kushinikiza serikali kumaliza matatizo yao ya posho na mishara.

HALI YA MAMBO ILIVYO NCHINI (DRIVING FORCES)
  • Ugumu wa maisha kutokana na kupanda kwa bei na gharama za maisha.
  • Maamuzi yasiyo na mashiko hasa kuongezeka kwa posho za wabunge.
SIDE EFFECTS
Wanaoumia ni wagonjwa wanaokosa huduma za kitabibu kutokana na mgomo huu. Serikali inapaswa kuchukua hatua za dharura kuokoa maisha ya wapiga kura wake hawa wanaokufa kutokana na ukosefu wa huduma.

FALACY: Imezoeleka miongoni mwa Watanzania kuwa Udaktari ni kazi ya wito, lakini si vema kutumia msemo huu kama nyundo ya kuvunjilia mbali juhudi zao za kutaka kufaidi matunda ya taaluma yao waliosota nayo shuleni kwa miaka mingi na pia juhudi zao kutaka kuishi maisha bora yenye thamani katika siku hizi ambazo hali ya uchumi imekuwa mbaya.

NINI KIFANYIKE?
Kugoma ni haki ya msingi ya binadamu yeyote mwenye timamu. Ufumbuzi wa Mgogoro huu unahusisha pande mbili tu ambazo ni Serikali na Madaktari. Hawa ndio wadau muhimu wa kuleta utatuzi wa mgogoro huu na hatimaye kupunguza madhara kwa pande ya tatu ambayo ni wagonjwa wanaoathirika kutokana na ukosefu wa HUDUMA.

KAULI MBIU YANGU.
  • Madaktari wasikilizwe na kutatuliwa matatizo yao
  • Usemi wa 'serikali sikivu' utafsiriwe kwa vitendo.
  • Wagonjwa mahospitalini wahudumiwe vema.



No comments:

Post a Comment